LOGO

Walisema ni fowadi mzigo? Leo watafunga midomo baada ya mshambuliaji Danny Welbeck kufunga mabao matatu ‘hat trick’ katika ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Galatasaray ya Uturuki.
Katika mechi hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya makundi iliyopigwa ndani ya Emirates, bao jingine la Arsenal lilifungwa na Alexis Sanchez.
Welbeck aliyejiunga na Arsenal akitokea Man United, alipiga mabao mawili, Sanchez akaongeza la nne.
Galatasaray walipata bao la kwa mkwaju wa penalti baada ya kipa wa Arsenal kufanya faulo na kulambwa kadi nyekundu.
Pamoja na ushindi, Arsenal waliendelea kuonyesha kupania kufunga mabao zaidi ingawa walipotea nafasi kadhaa.
Wakati Arsenal wanaibuka na ushindi mnono wakiwa nyumbani, Liverpool ambao wamerejea kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya walilala kwa bao 1-0 dhidi ya Basel wakiwa ugenini Uswiss.
Mshambuliaji wake, Mario Balotelli alishindwa kuonyesha kiwango huku Marco Streller akiwaua kwa bao pekee katika dakika ya 52.

MATOKEO MENGINE YA UEFA CHAMPIONS LEAGUE
FC BASEL 1-0 LIVERPOOL
ATLETICO MADRID 1- 0 JUVENTUS
REAL MADRID 2-1 LUDOGORETS RAZGRAD
ARSENAL 4-1 GALATASARAY
RSC ANDERLECHT 0-3 BORUSIA DORTUMUND
ZENIT ST PERTSBURG  0-0 AS MONACO
BAYER 04 LIVERKUSEN  3-1 BENFICA
MALMO 2-1 OLYMPIACOS

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top