
JUMAMOSI ndio Siku ambayo Vigogo wa Soka huko Spain, Real Madrid na FC Barcelona, watakapocheza Mechi yao ya kwanza ya La Liga Msimu huu Uwanjani Santiago Bernabeu kwenye pambano ambalo hubatizwa Jina rasmi ‘El Clasico.’
DONDOO MUHIMU:
-MFUNGAJI BORA DHIDI YA KIPA BORA: RONALDO v BRAVO!!
Msimu huu, Cristiano Ronaldo ameshapiga Bao 15 katika Mechi 7 za La Liga na anakutana na Kipa wa Barcelona Claudio Bravo ambae hajafungwa hata Bao 1 katika Mechi 7 za La Liga.
RONALDO ATAMTOBOA BRAVO?
-LUIS SUAREZ: KUCHEZA!
Meneja wa Barcelona, Luis Enrique, ametoboa kuwa Luis Suarez atacheza Mechi yake ya kwanza ya La Liga baada ya kumaliza Kifungo chake cha Miezi Minne lakini Meneja huyo amekataa kusema kama Straika huyo wa Urguay ataanza Mechi hiyo.
Safari
hii, licha ya kuwapambanisha wale Masupastaa bora Duniani, Cristano
Ronaldo, ambae ndiie rasmi Mchezaji Bora Duniani, na Lionel Messi, pia
atakuwepo Mfungaji Bora Duniani, James Rodriguez, alietwaa Buti ya
Dhahabu ya Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil, akiichezea Real Madrid
katika El Clasico yake ya kwanza.
Kivutio
kingine, akicheza El Clasico yake ya kwanza, ni Straika mpya wa
Barcelona, Luis Suarez, ambae hii huenda ikawa ni Mechi yake ya kwanza
rasmi kuichezea Barca baada ya kumaliza Kifungo chake cha Miezi Minne
alichopewa huko Brazil Mwezi Juni baada ya kumng’ata Beki wa Italy,
Giorgio Chellieni, kwenye Mechi ya Fainali za Kombe la Dunia.
Pia
Barca watatinga kwenye Mechi hii wakiwa chini ya Meneja mpya, Luis
Enrique, alietwaa wadhifa mwishoni mwa Msimu uliopita baada ya
kutimuliwa Gerardo Martino ambae aliiongoza Barca kumaliza Msimu
uliopita wakiwa kapa bila Kombe lolote.
Uso kwa Uso
-Jumla Mechi: 227
-Real Madrid Ushindi: 91
-Sare: 48
-Barcelona Ushindi: 88
Real
Madrid wao wamebaki na Meneja wao yule yule Mtaliana Carlo Ancelotti
ambae Msimu uliopita aliiwezesha Real kutwaa Copa del Rey kwa kuifunga
Barca 2-1 na pia kutwaa UEFA CHAMPIONZ LIGI baada ya kuwabonda Mabingwa
wa Spain, Atletico Madrid, Bao 4-1 kwenye Fainali.
Jumamosi,
Real watamkosa Mchezaji wao wa Bei ghali Duniani, Gareth Bale, ambae
ameumia Musuli za Mguu zilizomfanya pia aikose Mechi ya Kundi lao la
UEFA CHAMPIONZ LIGI waliyocheza Jumatano Usiku na kuichapa Liverpool 3-0
huko Anfield.
Kila
Timu ina Wachezaji wapya ambao huenda wakacheza hii El Clasico na
miongoni mwa hao ni pamoja na Jeremy Mathieu na Claudio Bravo wa Barca
wakati Real wanae James Rodriguez na Toni Kroos.
Hadi
sasa, baada ya Mechi 8, Barca wako kileleni mwa La Liga wakiwa na
Pointi 8 na Real wapo Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 4 nyuma yao huku Nafasi
ya Pili ikishikwa na Sevilla wenye Pointi 19 wakati Mabingwa Watetezi
Atletico Madrid wakiwa Nafasi ya 5 wakiwa na Pointi 17.
VIKOSI VINATARAJIWA:
Real Madrid: Casillas; Pepe, Sergio Ramos, Varane, Carvajal; Kroos, Modric, Rodriguez; Ronaldo, Benzema, Isco
Barcelona: Bravo; Pique, Alba, Alves, Mathieu; Mascherano, Iniesta, Xavi; Messi, Suarez, Neymar
MSIMAMO-Timu za Juu:
NA
|
TIMU
|
P
|
W
|
D
|
L
|
F
|
A
|
GD
|
PTS
|
1
|
FC Barcelona
|
8
|
7
|
1
|
0
|
22
|
0
|
22
|
22
|
2
|
Sevilla FC
|
8
|
6
|
1
|
1
|
15
|
8
|
7
|
19
|
3
|
Real Madrid CF
|
8
|
6
|
0
|
2
|
30
|
9
|
21
|
18
|
4
|
Valencia
|
8
|
5
|
2
|
1
|
17
|
7
|
10
|
17
|
5
|
Atletico de Madrid
|
8
|
5
|
2
|
1
|
14
|
7
|
7
|
17
|
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni