LOGO

 Cristiano Ronaldo and Gareth Bale celebrate after the Portuguese scored his second in the 5-1 victory
MABINGWA wa Ulaya, Real Madrid, Jumanne Usiku walikuwa kwao Santiago Bernabeu na kucheza Mechi ya La Liga na Elche CF na kuitwanga Bao 5-1 huku Mchezaji Bora Duniani Cristiano Ronaldo akipiga Bao 4.
Hii ni Mechi ya Pili mfululizo kwa Real kushinda kwa kishindo baada ya Jumamosi kuichakaza Deportivo La Coruna Bao 8-2.
Elche CF walitangulia kufunga kwa Penati ya Dakika ya 15 aliyopiga Edu Albacar na Real kujibu mapigo kwa Bao za Gareth Bale, Dakika ya 20, na za Cristiano Ronaldo, Dakika ya 28 kwa Penati na Dakika ya 32.
 
Hadi Mapumziko, Real 3 Elche 1.
Kipindi cha Pili, Ronaldo alipiga Bao lake la 3 la Mechi na la 4 kwa Real baada ya yeye mwenyewe kuangushwa ndani ya Boksi na Pašalić na kuamriwa Penati aliyofunga.
Hiyo ni Hetitriki ya 25 kwa Klabu yake Real na kwenye La Liga, Ronaldo amefikisha Hetitriki 21 na amebakisha 1 tu kufikia Rekodi inayoshikiliwa kwa pamoja na Alfredo Di Stefano na Straika wa Athletic Club, Telmo Zarra, katika Historia ya La Liga.
Dakika ya 92, Ronaldo alipiga Bao lake la 4 kwa Mechi hii na kuipa Real ushindi wa Bao 5-1.
La Liga itaendelea Jumatano Usiku ambapo Vinara, FC Barcelona, na Mabingwa Watetezi, Atletico Madrid, wote watakuwa Ugenini.
 Real Madrid players celebrate with Ronaldo en route to victory in front of their home fans
VIKOSI:
Real Madrid (4-3-3): Keylor Navas; Carvajal, Varane, Ramos, Marcelo; Illarramendi, Kroos, Isco; James, Ronaldo, Bale.
Akiba: Casillas,  Arbeloa, Nacho, Fábio Coentrão, L. Modrić, K. Benzema, J. Hernández
Elche (4-3-3): Manu Herrera; Cisma, Lomban, Pelegrín, Albacar; Mosquera, Víctor, Adrian; Rodrigues, Jonathas, Coro.
Akiba: P. Tytoń, José Ángel, D. Suárez, E. Roco, M. Pašalić, F. Fajr, Cristian Herrera
Refa: Carlos Clos Gomez

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top