LOGO

 
Wakicheza kwao Old Trafford, Manchester United wameifunga West Ham Bao 2-1 katika Mechi ya Ligi Kuu England na kukwea hadi Nafasi ya 7 lakini watamkosa Nahodha wao Wayne Rooney kwa Mechi 3 zijazo baada ya kutwangwa Kadi Nyekundu.
Hadi Mapumziko Man United walikuwa mbele kwa Bao 2-1 kwa Bao za Nahodha Wayne Rooney, ambae sasa ametimiza Miaka 10 akiwa Old Trafford,  baada kuunganisha pande safi la Rafael katika Dakika ya 5 na Robin van Persie kupiga Bao la Pili katika Dakika ya 22 baada ya kazi njema ya Ander Herrera na Radamel Falcao.
West Ham walifunga Goli lao baada ya kutokea kizaazaa kufuatia Kona na Diafra Salho kukwamisha Mpira wavuni katika Dakika ya 37.
Dakika ya 54 Man United walibakia Mtu 10 baada ya Refa Lee Mason kumpa Kadi Nyekundu Nahodha Wayne Rooney kwa madai amemchezea Rafu mbaya Stewart Downing.
Hii inamaanisha Rooney atazikosa Mechi 3 za Timu yake dhidi ya Everton,WBA na Chelsea.
Tukio hilo liliwafanya Man United wamtoe Straika Falcao na kumwingiza Kiungo Darren Fletcher.
Katika Mechi hii, Man United walimchezesha Kina wa Miaka 19 kutoka Timu ya Rizevu, Paddy  McNair kama Sentahafu akishirikiana na Marcos Rojos na Kijana huyo alisimama imara.
 
VIKOSI:
MAN UNITED: De Gea, Rafael, McNair, Rojo, Shaw, Blind, Herrera, Di Maria, Rooney, van Persie, Falcao
Akiba: Lindegaard, Thorpe, Fletcher, A Pereira, Valencia, Mata, Januzaj. Akiba:
WEST HAM: Adrian, Reid, Cresswell, Tomkins, Downing, Sakho, Demel, Amalfitano, Poyet, Song, Valencia
Akiba: Jaaskelainen, Nolan, Zarate, Vaz Te, Jenkinson, Collins, Cole
REFA: Lee Mason

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top