
Mashabiki wa timu ya ndanda fc ya Mkoani Mtwara wanaondoka usiku wa leo kuelekea mkoani Shinyanga kwenda kuiunga mkono timu yao ya Ndanda Fc inaposhuka dimbani hapo keshokutwa katika dimba la kambarage kumenyana na timu ya Stand United katika mchezo wa ufunzi wa ligi kuu Tanzania Bara. Mashabiki hao wakiongozwa na mwenyekiti wa kundi hilo Salumu mabomba wamehamasika na kuwa na imani na timu yao ya Ndanda ambayo septemba 13 walitoka suluhu na Simba katika mchezo wao wa kirafiki wa maadhimisho ya siku ya ndanda, hivyo iliwapa moyo wapenzi na mashabiki hao. Mashabaki hao walikuwa wakikutana kila mwishoni mwa wiki kupanga mikakati na kila mwanachama kutoa mchango wa sh 3000, kwa kila mshabiki kwa ajili ya nauli ya kusafili na timu hiyo kila inakokwena kucheza mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara abayo inaanza kutimua vumbi hapo kesho. “Tunaondoka usiku huu wa ijumaa kuelekea Shinyanga tayali Vijana wanahamasa kubwa na tupo katika maandalizi ya mwisho na kutokana na timu yetu kutuoneshakwamba imedhamilia kuhakikisha inatuwakilisha vizuri basin a sisi lazima tusiwavunje moyo lazima tuwapatie ushirikiano wa kutosha ili waweze kutimiza dhamira yao” alisema Mabomba. Alisema kuwa baadhi ya wadau wamejitokeza na kuwapatia nguvu kwa swala la usafiri hivyo wamewashukuru waendelee kuwa na moyo kama huo na wale ambao wako tayari kuisaidia timu hiyo ili iweze kufanya vizuri wanaombwa kujitokeza hata kwa kitu chochote kwa mashabiki hao ambao wameamua kujitoa kwa ajili ya kuiunga mkono timu hiyo. “Tunajuwa kama mashabiki tunasafari ndefu ya kuhakikisha timu yetu tunainga mkona na iweze kufanya vizuri, ili swala hili lisikwame ni lazima watuunge mkono kwa kutuwezesha kiasi cha pesa au usafiri wa kufika kila inapocheza timu yetu kwani sisi wenyewe toka timu hiyo ipande daraja tulikuwa tukichangia sh 3000 kila wiki ila pasha hiyo haiwezi kutosha kutufikisha michezo yote ya nje” alisema kiongozi huyo wa kundi hilo maarufu kama Ndanda kwa Roho safi. Ndanda Fc inayonolewa na kocha mzawa Denis Kitambi, ilipanda daraja msimu huu katika ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara ikiungana na Stand united ya mjini shinyanga na Polisi ya Morogoro ambazo nazo zimepanda daraja msimu huu. Ndanda keshokutwa inashuka dimbani katika uwanja wa kambarage mjini shinyanga wakiwa wageni wa Stand united, katika mechi ya kwanza ya ufunguzi wa ligi kuu ya vodakomu Tanzania bara kwa msimu wa 2014/2015.
SHAFFIHDAUDA
MASHABIKI NDANDA KUWASILI SHINYANGA LEO. Kitaifa
NA BARAKA JAMALIMTWARA
Mashabiki wa timu ya ndanda fc ya Mkoani Mtwara wanaondoka usiku wa leo kuelekea mkoani Shinyanga kwenda kuiunga mkono timu yao ya Ndanda Fc inaposhuka dimbani hapo keshokutwa katika dimba la kambarage kumenyana na timu ya Stand United katika mchezo wa ufunzi wa ligi kuu Tanzania Bara.
Mashabiki hao wakiongozwa na mwenyekiti wa kundi hilo Salumu mabomba wamehamasika na kuwa na imani na timu yao ya Ndanda ambayo septemba 13 walitoka suluhu na Simba katika mchezo wao wa kirafiki wa maadhimisho ya siku ya ndanda, hivyo iliwapa moyo wapenzi na mashabiki hao.
Mashabaki hao walikuwa wakikutana kila mwishoni mwa wiki kupanga mikakati na kila mwanachama kutoa mchango wa sh 3000, kwa kila mshabiki kwa ajili ya nauli ya kusafili na timu hiyo kila inakokwena kucheza mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara abayo inaanza kutimua vumbi hapo kesho.
“Tunaondoka usiku huu wa ijumaa kuelekea Shinyanga tayali Vijana wanahamasa kubwa na tupo katika maandalizi ya mwisho na kutokana na timu yetu kutuoneshakwamba imedhamilia kuhakikisha inatuwakilisha vizuri basin a sisi lazima tusiwavunje moyo lazima tuwapatie ushirikiano wa kutosha ili waweze kutimiza dhamira yao” alisema Mabomba.
Alisema kuwa baadhi ya wadau wamejitokeza na kuwapatia nguvu kwa swala la usafiri hivyo wamewashukuru waendelee kuwa na moyo kama huo na wale ambao wako tayari kuisaidia timu hiyo ili iweze kufanya vizuri wanaombwa kujitokeza hata kwa kitu chochote kwa mashabiki hao ambao wameamua kujitoa kwa ajili ya kuiunga mkono timu hiyo.
“Tunajuwa kama mashabiki tunasafari ndefu ya kuhakikisha timu yetu tunainga mkona na iweze kufanya vizuri, ili swala hili lisikwame ni lazima watuunge mkono kwa kutuwezesha kiasi cha pesa au usafiri wa kufika kila inapocheza timu yetu kwani sisi wenyewe toka timu hiyo ipande daraja tulikuwa tukichangia sh 3000 kila wiki ila pasha hiyo haiwezi kutosha kutufikisha michezo yote ya nje” alisema kiongozi huyo wa kundi hilo maarufu kama Ndanda kwa Roho safi.
Ndanda Fc inayonolewa na kocha mzawa Denis Kitambi, ilipanda daraja msimu huu katika ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara ikiungana na Stand united ya mjini shinyanga na Polisi ya Morogoro ambazo nazo zimepanda daraja msimu huu.
Ndanda keshokutwa inashuka dimbani katika uwanja wa kambarage mjini shinyanga wakiwa wageni wa Stand united, katika mechi ya kwanza ya ufunguzi wa ligi kuu ya vodakomu Tanzania bara kwa msimu wa 2014/2015.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni