LOGO

 
Hatimaye mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi amepata kibali cha muda cha kufanya kazi nchini ambacho kitamwezesha kuichezea klabu ya Simba.  Kutolewa kwa kibali hicho, kunafanya idadi ya wachezaji wa kigeni wa Wekundu hao wa  Msimbazi, kufikia watatu baada Idara ya Uhamiaji kufanya hivyo kwa wachezaji wawili; Mrundi Pierre Kwizera na Mkenya Paul Kiongera. Mwingine aliyepata kibali ni kocha wa timu hiyo, Patrick Phiri.  Wengine ambao hawajapata kibali ni Amissi Tambwe na Joseph Owino.  Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe alisema jana kuwa baada ya kufuatilia, wamegundua Okwi tayari alikuwa na kibali kingine cha kufanya kazi Yanga.  “Tumefanikiwa kupata kibali cha muda kwanza, baada ya leo tutafanya utaratibu wa kuwasiliana na ndugu zetu Yanga, ili waandike barua ya kwamba Okwi si mfanyakazi wao tena ili sisi tuweze kupatiwa kibali chake kamili,” alisema Hans Poppe.  Hata hivyo, huenda Simba ikapata mtihani mgumu katika mpango huo kutokana na sakata la mshambuliaji huyo na Yanga.  Klabu hiyo ya Jangwani haijafuta nia yake ya kumshtaki Okwi Fifa huku ikipinga uamuzi ya Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya TFF kumwidhinisha kuchezea Simba.

MWANANCHI

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top