Moto mkubwa umetekeza makao ya shirikisho la soka la Nigeria NFF iliyoko Abuja.
Iliwachukua zaidi ya saa mbili kwa zima moto wakisaidiana na umma kuuzima moto huo mkubwa .Katibu mkuu wa NFF bwana Musa Amadu amesema kuwa moto huo ulianzia katika afisi ya mhasibu wa shirikisho hilo.
"Niliwasili kama kawaida lakini nikakatazwa kupanda ghorofa kwani tayari moshi ulikuwa unafuka ''
"Wafanyikazi wa shirikisho hilo wangeweza kuzima moto huo lakini walishindwa kuingia ofisini humo na hivyo hawangfeweza kubaini chanzo kikamilifu''
''Hata hivyo nashukuru mungu kuwa hakuna mtu aliyepoteza maisha yake kutokana na moto huo kwahivyo hakuna faida ya kumlaumu mtu yeyote''
Mabingwa hao wa Afrika hawana kocha hata kufikia sasa .
Afisi iliyoko sasa ingali haijatia sahihi makubaliano yeyote wala kandarasi na aliyekuwa kocha wa timu hiyo Stephen Keshi ambaye aliiongoza timu hiyo kuenda kwenye kombe la dunia huko Brazil.
Keshi mwenyewe ameiambia BBC kuwa anatarajia kukamilisha mazungumzo kati ya saa 24 hadi 48 zijazo.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni