AZAM
FC kesho itacheza mechi yake ya mwisho ya Kundi A, Klabu Bingwa Afrika
Mashariki na Kati, Kombe la Kagame dhidi ya Adama City ya Ethiopia bila
beki aliye katika kiwango cha juu hivi sasa, Shomary Kapombe.
Mchezaji huyo wa zamani wa AS Cannes ya Ufaransa na Simba SC ya Tanzania pia, anasumbuliwa na nyama za paja na siku ya pili leo ameshindwa kufanya mazoezi na wenzake.
Mchezaji huyo wa zamani wa AS Cannes ya Ufaransa na Simba SC ya Tanzania pia, anasumbuliwa na nyama za paja na siku ya pili leo ameshindwa kufanya mazoezi na wenzake.
Kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog ameithibiishia ni kweli, Kapombe hatakuwepo kabisa katika mchezo wa kesho, wakati mshambuliaji Mhaiti, Leonel Saint- Preux ambaye pia yupo vizuri, naye atakosekana- wote wakiwa wanasumbuliwa na maumivu ya nyama za paja.
Nahodha John Bocco ‘Adebayor’ aliyekosa mechi ya sare ya 2-2 na Atlabara ya Sudan Kusini, amefanya mazoezi jana na leo- maana yake kesho anaweza kurudi uwanjani.
Atlabara yenye pointi tatu na Adama pointi mbili, zote zinataka kushinda kesho Uwanja wa Nyamirambo ili kuchukua nafasi ya tatu katika kundi hilo, ziweze kuungana na Azam na Rayon kwenda Robo Fainali.
bin zubeiry
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni