PITIA:
MENEJA wa Manchester United Louis van Gaal:
"Inasikitisha tumefungwa Mechi yetu ya kwanza nyumbani. Hatukufikia kwenye kiwango tunachoweza kucheza. Hilo linasikitisha kwani tuna uwezo wa kucheza zaidi ya hapo lakini ukishindwa kufanya hivyo nyumbani inasikitisha hasa kwa Mashabiki wako. Tulikuwa na mchecheto hasa Kipindi cha Kwanza. Kipindi cha Pili hatukucheza kama Timu na kwa hilo nawajibika. Tulipata nafasi nyingi kupita Swansea lakini hilo halisemi lolote kuhusu matokeo. Ni Magoli ndio muhimu. Ilipokuwa 1-1 nilihisi tutashinda lakini kwa sababu hatukucheza Kitimu tulikuwa tukifanya makosa wakati tukienda mbele kushambulia. Wachezaji walijitahidi lakini wanatakiwa wacheze Kitimu kufikia kiwango chao.”
DONDOO:
-Mara ya mwisho Manchester United kuanza Msimu mpya na kufungwa Nyumbani kwao Old Trafford ni Msimu wa 1972/73 walipofungwa 3-2 na Ipswich Town!
-MENEJA wa Swansea Garry Monk:
"Kabla ya Msimu kuanza tulifanya kazi kubwa kuimarisha uchezaji wetu kwenye Difensi na hili limetusaidia hii Leo dhidi ya Timu nzuri Manchester United hasa baada ya kufunga Magoli."
Danny Mills, Mchambuzi wa BBC Radio 5:
"Wako mbali na UEFA CHAMPIONZ LIGI. Nimeshafanya Utabiri wangu kwamba watamaliza Nafasi ya 5 kwenye Ligi ikiwa watapata Wachezaji wapya. Timu haina Wachezaji wazuri. Ukiwaondoa Wayne Rooney, Robin van Persie na Juan Mata, nani yupo? Ed Woodward alipondwa sana Msimu uliopitwa kwa kutoleta Wachezaji wapya. Na safari hii tena watafanya kosa hilo hilo?"
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni