AZAM
FC imepunguzwa kasi katika Kombe la Kagame, baada ya kulazimishwa sare
ya mabao 2-2 na Atlabara ya Sudan Kusini jioni hii Uwanja wa Stade de
Kigali, Nyamirambo mjini hapa.
Mshambuliaji
wa zamani wa Yanga SC, Didier Kavumbangu aliinusuru Azam kuzama katika
mchezo huo wa Kundi A Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, baada ya
kuifungia bao la kusawazisha dakika ya 86, baada ya krosi ya Shomary
Kapombe.Azam
ilikwenda kupumzika ikiwa inaongoza kwa bao 1-0 lililofungwa na kiungo
Kipre Michael Balou kwa shuti la mpira wa adhabu kutoka umbali wa mita
20, baada ya pacha wake, Kipre Herman Tchetche kuangushwa.
Atlabara
ilirudi vizuri kipindi cha pili na kufanikiwa kusawazisha bao dakika ya
48, mfungaji Nahodha wake, Thomas Batista kabla ya kufunga la pili
dakika ya 60 mfungaji Bony Martin.
Atlabara ilipata pigo dakika ya 89 baada ya Nahodha wake, Batista kutolewa nje kwa kadi nyekundu.
Kwa
matokeo hayo, Azam inafikisha pointi tano baada ya mechi tatu na
kujihakikishia nafasi ya kwenda Robo Fainali ya michuano hiyo, wakati
Atlabara inafikisha pointi mbili baada ya mechi mbili.
Kikosi
cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Gardiel Michael, Shomary Kapombe,
Said Mourad, Aggrey Morris, Kipre Balou, Himid Mao, Salum Abubakar ‘Sure
Boy’, Gaudence Mwaikimba/Didier Kavumbangu dk63, Leonel Saint Preux na
Kipre Tchetche/Khamis Mcha dk63.
Atlabara;
Jacko Mpenzi, Thomas Batista, Hamza Olema, Hatit Monydeng, Ibrahim
Sebit, Kharim Mutawakil, Frando Justin Wani, Joseph Aquer, Dak
Kujbor/Khamis Leon dk56 na Bony Martin.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
ZILIZOSOMWA SANA
-
MICHUANO ya kombe la Mapinduzi 2015 iliyoanza kutimua vumbi jana inatarajia kuendelea tena leo kwa mitanange mitatu kupig...
-
Nahodha wa Liverpool Steven Gerrard ametangaza kuwa ataondoka Liverpool mwishoni mwa msimu huu baada ya kudumu liverpool kwa kipindi cha mi...
-
Siku kadhaa baada ya Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), kuifungia Kampuni ya Lino International kuendesha mashindano ya Miss Tanzani...
-
LIGI KUU ENGLAND Wikiendi hii inaanza kwa Mechi ya Jumamosi ya mapema kabisa huko...
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni