LOGO

 Mbwana Samata (kushoto) na Thomas Ulimwengu wakishangilia goli la pili lililofungwa na Ulimwengu
Siku moja tu baada ya kuanza Mkataba wa kudumu kuwa Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Charles Boniface Mkwasa ameanza vyema himaya yake baada ya kuichapa Malawi Bao 2-0 katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Kwanza ya Mechi za Mchujo kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Urusi.
Bao zote za Tanzania zilifungwa Kipindi cha Kwanza na Wachezaji Maprofeshenali wanaocheza huko Lubumbashi, Congo DR kwenye Klabu ya TP Mazembe, Mbwana Samatta, Dakika ya 18, na Thomas Ulimwengu, Dakika ya 22.
Jumapili Tanzania itarudiana na Malawi huko Blantryre Nchini Malawi na Mshindi atasonga Raundi ya Pili na kucheza na Algeria Mwezi Novemba.
VIKOSI:
Tanzania: Mustapha, Shomari Kapombe, Mwinyi Haji, Nadir Haroub, Kevin Yondani, Himid Mao , Said Ndemla, Farid Mussa, Thomas Ulimwengu, Mrisho Ngassa, Mbwana Samatta
Akiba: Aishi Manula, Salum Telela, Mohamed Hussein, Hassan Isihaka, Mudathir Yahya, Simon Msuva, Ibrahim Hajib.
Malawi: Simplex, Sanudi, Gabeya, Fadya, Mzava, Phiri, Kayira, Mhone, Kawanda, Banda, Ngalande

Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la Hereniko Mashiku and +255653442672 kwa matangazo

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top