Pata nini kimejiri kwenye Klabu hizo:
DAVID DE GEA AKATWA MAN UNITED!
Kipa waManchester United David De Gea hatacheza dhidi ya Tottenham hapo Kesho huku akiendelea kuhusishwa na kuhamia Real Madrid.
Kwa kipindi chote hiki kuelekea Msimu mpya ambao unaanza Kesho kwa hiyo Mechi Uwanjani Old Trafford, De Gea, mwenye Miaka 24, ametajwa sana kutaka kurudi kwao Spain kuichezea Real.
Akiongelea Mechi hii ya kwanza, Meneja wa Man United, Louis van Gaal, amesema: “Namfikiria yeye kama binadamu na si Mchezaji. Naona hatamudu haya.”
Kukosekana kwa De Gea kunaweza kufungua njia kwa Kipa mpya wa Kimataifa wa Argentina, Sergio Ramos, kucheza Mechi yake ya kwanza kabisa.
Kipa mwingine wa Man United ni Kipa wa zamani wa Barcelona, Victor Valdes, mwenye Miaka 33, lakini nae ametemwa kwenye Kikosi cha Kwanza na yumo kwenye Listi ya Wachezaji wanaouzwa baada ya kufarakana na Van Gaal.
MANUEL PELLEGRINI ASAINI MKATABA MPYA MAN CITY!
Meneja wa Manchester City Manuel Pellegrini amesaini Mkataba mpya utakaomweka huko Etihad hadi 2017.
Mkataba wake wa awali ulitakiwa kumalizika Mwakani baada ya kuteuliwa Meneja wa Man City Juni 2013 kumrithi Roberto Mancini.
Sambamba na Pellegrini, Wasaidi wake pia wamepewa nyongeza za Mikataba yao na hao ni Meneja Msaidizi Ruben Cousillas, Kocha wa Makipa Xabier Mancisidor na Kocha wa Viungo Jose Cabello.
Man City wanaanza Msimu wao mpya kwenye Ligi Kuu England kwa kucheza Ugenini na West Brom hapo Jumatatu.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni