Klabu
za Manchester City na Swansea City zimefikia muafaka wa kuuziana
mchezaji Wilfried Bonny kwa ada inayotajwa kufikia paundi milioni 30.
Kwa
mujibu wa gazeti la The Mirror la nchini Uingereza limeandika kuwa
vilabu hivyo viwili tayari vimekwisha kubaliana kwenye mambo ya msingi
kuhusiana na mauzo ya mchezaji huyo na kinachosubiriwa sasa ni
makubaliano binafsi tu baina ya Man City na Bonny.
Taarifa
zinadai kuwamchezaji huyo raia wa Ivory Coast anatarajiwa kusaini
mkataba wa miaka minne ambao atakua akijikusanyia kiasi cha paundi
100,000 kwa wiki kama mshahara wake mara baada ya kuvuja jasho klabuni
hapo.
Ikumbukwe
tayari mchezaji huyo alisha waalifu mabosi wa klabu yake hiyo kuwa
anataka kucheza ligi ya mabingwa barani Ulaya na hivyo itakapotokea kuwa
kuna timu inayoshirki michuano hiyo basi ofa hiyo ifikiriwe zaidi.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni