Simba sc imeingia kwenye hatua hiyo baada ya kumaliza akiwa kinara wa kundi C kwa kufikisha point 6 wakati Taifa jang'ombe wakiingia kwenye hatua hiyo kama bestloser wa pili baada ya jana kufanikiwa kutoa suluhu na polisi na shilingi ikaamua Taifa jang'ombe ipite kama best loser wa pili na polisi wakipita akiwa nafasi ya pili.
Utumiaji wa shilingi ulitumika baada ya Polisi na Taifa jang'ombe kulikana kwa kila kitu, wakiwa wamefungwa goli 4 kila mmoja na kila mmoja akishinda goli moja na huku wote wakifikisha point 4.
Michezo mingine ya robo fainali itachezwa kesho ambapo KCCA watafunguwa na Polisi saa 9 alasiri, Azam fc watakabiliana na Mtibwa sugar saa 11 jioni na mchezo wa mwisho utakaochezwa 2 usiku utakuwa kati ya yanga na JKU.
Katika hatua nyingine jana Yanga walifanikiwa kupata ushindi wa 3 baada ya kuwafunga Shaba goli 1-0 goli lililopatikana katika dakika ya 86 kupitia kwa Adrey Countinho akiunga krosi ya Msuva.
Katika mchezo huo yanga walipoteza nafasi kadhaa kupitia kwa Tambwe, Mrwanda, Ngassa na Msuva wakati Shaba wakipoteza nafasi mbili za kujipatia magoli.
Katika michezo ya awali hapo jana Azam fc waliwafunga mtende goli 1-0, goli lililofungwa na Kavumbagu huku KCCA wakiwa wachapa KMKM goli 2-1 na Taifa jang'ombe wakitoka suluhu (0-0) na polisi
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni