ZILE
mbio za Mechi 22 za Real Madrid bila kufungwa katika Mechi rasmi za
Mashindano Leo hii zimemalizika baada ya kufungwa 2-1 na Valencia huko
Estadio Mestalla katika Mechi yao ya kwanza ya La Liga kwa Mwaka 2015.
Cristiano
Ronaldo aliipa Real Bao la kuongoza wa Penati ya Dakika ya 14 lakini
Valencia wakapiga Bao 2 Kipindi cha Pili kupitia Antonio Barragan na
Nicolas Otamendi kuwapa Bao la ushindi.
Matokeo
hayo yamewabakisha Real Pointi 1 mbele ya Barcelona ambao wanaweza
kutwaa uongozi wakiifunga Real Sociedad baadae Leo hii ingawa Barca
watakuwa wamecheza Mechi 1 zaidi.
VIKOSI:
Valencia (Mfumo 3-4-1-2): Diego Alves; Orban, Otamendi, Mustafi; Barragan, Parejo, Enzo Perez, Piatti; Andre Gomes; Negredo, Alcacer.
Real Madrid (Mfumo 4-3-3): Casillas; Carvajal, Pepe, Sergio Ramos, Marcelo; Kroos, Isco, James Rodriguez; Bale, Ronaldo, Benzema.
REFA: Jesús Gil
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni