Huku zilizoshika nafasi nne za juu msimu uliopita wakipata shavu la lushiriki michuano ya Mapinduzi cup Zanzibar timu hizo ni Yanga, Simba, Azam
fc na Mtibwa Sugar haikuzuia kusimama kwa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara ambapo leo January 3 viwanja mbalimbali vitawaka moto kupisha mitanange hiyo.
Timu zitakazoingia uwanjani kwa mujibu wa ratiba ni Wagosi wa Kaya, Coastal Union watawakaribisha Maafande wa JKT Ruvu
katika mechi ya raundi ya 9 ya ligi kuu itakayopigwa uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga.
Wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao 1-0 katika
mechi iliyopita dhidi ya JKT Ruvu, Maafande
wa Ruvu Shootings watawaalika ‘Wanankurukumbi’ Kagera Sugar FC kwenye uwanja wa
Mabatini Mlandizi mkoani Pwani.
Kagera Sugar waliomfukuzisha kazi kocha wa Simba,
Mzambia Patrick Ackson Phiri watakuwa ugenini kwa lengo la kuendeleza dozi yao.
Polisi Morogoro watakabiliana na Stand United
katika uwanja wa michezo wa Jamhuri uliopo mjini Morogoro.
Jumapili januari 4 mwaka huu, Nyasi za uwanja wa
CCM Sokoine zitawaka moto kwa wenyeji Tanzania Prisons, ‘Wajelajela’ kuchuana
na Ndanda fc.
Mechi baina ya Mbeya City fc na Yanga, Azam fc
dhidi ya Mtibwa Sugar pamoja na ile ya Mgambo na Simba zimeahirishwa kwani Yanga,
Simba, Azam na Mtibwa zipo Zanzibar.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni