LOGO

Liverpool forward Raheem Sterling is set to agree a new five-year contract worth £100,000-a-week
Timu ya Liverpool imekubali kumpa mkataba mpya winga wa timu hiyo Raheem Sterling, mkataba huo utakuwa na thamani ya pauni milioni 25 huku mchezaji huyo akitarajiwa kupokea mshahara wa kiasi cha pauni 100,000 kwa wiki katika mkataba huo ambao utakuwa wa miaka mitano.

Sterling ambaye ana miaka 20 bado ana miaka miwili zaidi kwenye mkataba wake wa zamani lakini timu ya Liverpool haitaki kumpoteza mchezaji huyo baada ya timu za Real Madrid na Manchester City kuonyesha kutaka kumsajili.

Liverpool ambayo ilimsajili mchezaji huyo kutoka QPR mwaka 2010 akiwa na miaka 15 imekuwa ikimtumia Sterling kama mshambuliaji kwa mechi nyingi za ligi kuu nchini Uingereza hasa baada ya kuumia kwa Daniel Sturridge na Mario Balotelli kushindwa kuiongoza vyema safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.

Baada ya nahodha wa timu hiyo Steven Gerrard kutangaza kwamba ataiacha timu hiyo mwishoni mwa msimu uongozi wa klabu ya Liverpool hauitaji kumpoteza mchezaji mwingine na ndiyo maana Raheem anatarajiwa kupewa mkataba huo mnono.

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top