LOGO

 
Mchezo wa kombe la mapinduzi wa kundi C ulio wakutanisha vinara wa ligi kuu ya Zanzibar JKU dhidi ya vinara wa ligi kuu ya Tanzania bara Mtibwa sugar ulimalizika kwa sare ya goli 1-1.
Katika mchezo huo ambao Mtibwa sugar walianza na wachezaji wawili walioanza katika mchezo wa kwanza walioshinda dhidi ya simba sc na wachezaji wengine 9 wakiwa benchi.

Mtibwa sugar ndio walikuwa wa mwanzo kuandika goli kupitia kwa Mussa Hassan Mgosi dakika ya 20 na goli hilo kudumu kwa dakika 45 za kwanza na mtibwa sugar wakienda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 1.

Katika kipindi cha pili JKU walionekana kuwa vizuri kulinganisha na mtibwa sugar ambapo katika dakika ya 72 walifanikiwa kupata goli la kusawazisha kupitia kwa Amour Omary ikiwa ni baada ya mtibwa sugar kupoteza penati kupitia kwa Mgosi katika dakika ya 53.

Kwa matokeo hayo ya sare JKU na Mtibwa sugar wamefikisha point 4 na wanakalia katika uongozi wa kundi C.

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top