LOGO

Kagera Sugar imeshindwa kuifunga Ruvu Shooting leo kwenye mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Mabatini, baada ya kutoka sare ya bila magoli yani 0-0 huku timu zote zikicheza kwa ustadi mkubwa.  Kwa upande wa Ruvu Shooting, wao wamepeleka lawaza zao kwa mwamuzi wa mchezo huo na kudai kuwa walistahili kupata penalty kupitia msemaji wa klabu hiyo, Masau Bwire.
Kagera ambao mechi iliyopita walitoka kuwalaza wekundi wa Msimbazi timu ya Simba kwa bao 1-0, matokeo hayo yanawafanya kuweza kutimiza alama 14 na sasa kuwa sawa kwa pointi na timu za Yanga na Azam licha ya wanankurunkumbi hao kuwa mbele kwa mchezo mmoja.
Ruvu Shooting ambao mechi iliyopita walipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ruvu JKT, sasa wametimiza alama 11 na mchezo unaofuata watasafiri hadi Tanga kwenda kucheza na timu ya Mgambo JKT kabla ya kwenda Dar es Salaam kuvaana na timu ya Yanga kwenye mzunguko wa 11.
Kwa upande wa Kagera Sugar, wao watarejea sasa nyumbani kuwasubiri mabingwa watetezi timu ya Azam kwenye dimba la Kaitaba na kwenye mzunguko wa 11, watasalia ndani ya Kaitaba kuwaalika Mbeya City kutoka Jijini Mbeya.

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top