LOGO


Vinara wa ligi kuu ya Tanzania Bara Mtibwa Sugar wanataraji hapo kesho kupima taa za uwanja wa Azam complex pale watakapo kabiliana na Azam FC katika uwanja huo unaomilikiwa na Azam fc.

Klabu ya Azam FC wamekuwa katika harakati ya kuhakikisha mechi zao za nyumbani zinachezwa usiku kuanzia msimu huu, japo katika michezo yake minne ya awali ya ligi kuu yavodacom walishindwa kucheza husuku kutokana na taa kutokuwa teyari kuhimili mikimiki ya usiku.

Kesho Azam FC watacheza na Mtibwa sugar katika mchezo wa kirafiki ambao utatumika vile vile katik kuzipima taa za uwanjani hapo, ikiwa ni mara ya kwanza kwa Azam FC kucheza usiku katika uwanja huo.

Mchezo huo wa kesho utaanza saa moja usiku na huenda ukarushwa moja kwa moja kupita kingamuzi cha Azam TV.

Azam FC baada ya mchezo huo wataelekea nchini Uganda kwa ajili ya michezo mitatu ya kirafiki ambapo mchezo wa kwanza watachezaji desemba 13.

Azam FC wako katika maandalizi ya kutetea taji la ligi kuu ya vodacom ambapo mpaka sasa ligi hiyo inaongozwa na Mtibwa Sugar wenye pointi 15, wakifuatiwa na Azam FC na anga wenye pointi 13 kila mmoja.

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top