LOGO

MOURINHOJose Mourinho anawagwaya ‘Papa wa Baharini’ wakati Chelsea ikisubiri kujua nani atakuwa Mpinzani wake kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, ambayo Droo yake itafanyika Jumatatu Desemba 15.
Chelsea waliibuka Vinara wa Kundi lao la UCL Jana Usiku baada ya kuichapa Sporting Lisbon Bao 3-1 Uwanjani Stamford Bridge.
Kwenye Droo hiyo Chelsea wanaweza kupambanishwa na mmoja kati ya Juventus, PSG, FC Basel, Bayer Leverkusen au Shakhtar Donetsk.
Akiongea hiyo Jana baada ya ushindi wao, Mourinho alisema: “Hatuogopi Mtu yeyote lakini tunajua zipo Timu nzuri na Timu kali kwenye Mashindano haya. Mwaka Jana tulikuwa karibu mno na hatukuwa na Timu inayocheza kiwango cha juu kama Msimu huu kwa hiyo tunaweza kuota tutafanikiwa.”

Arsenal:
-WANAWEZA KUCHEZA NA:
Atlético Madrid, Real Madrid, Monaco, Bayern, Barcelona, Porto
Manchester City FC:
-WANAWEZA KUCHEZA NA:
Atlético Madrid, Real Madrid, Monaco, Dortmund, Barcelona, Porto
Mourinho aliongeza: “Ngoja tuone kama tutanusurika na Papa kwa sababu wapo Papa Baharini!”
Hata hivyo, kwa Chelsea kumaliza kama Vinara wa Kundi lao, kwenye Droo wapo Chungu kimoja na Timu zilizomaliza Nafasi za 1 kwenye Makundi yao ambazo ni pamoja na Mabingwa Watetezi Real Madrid, Barcelona na Bayern Munich, na ambazo haziwezi kukutanishwa.
Pia, Timu toka Nchi moja na zile zilizotoka Kundi moja haziwezi kupambanishwa katika Raundi ya Mtoano ya Timu 16.
Hii inamaanisha Chelsea haiwezi kukutana na Aresnal pamoja na Manchester City ambao wako Chungu cha Pili baada kumaliza za Nafasi ya Pili kwenye Makundi yao na pia haiwezi kupewa Schalke ambao walikuwa nao Kundi moja.
Mourinho pia alikiri kuwa Timu zote kubwa huko Ulaya zipo labda Liverpool ambayo imetupwa nje kwa kumaliza Nafasi ya 3 kwenye Kundi lao na hivyo kupelekwa kucheza Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya EUROPA LIGI.

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top