Washindi wa Ngao ya Jamii msimu wa 2014/2015 timu ya Young Africans kesho asubuhi wanatarajia kuondoka jijini Dar es salaam kuelekea mjini Morogoro tayari kwa mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara dhidi ya wakata miwa Mtibwa Sugar katika dimba la Uwanja Jamhuri.
Kikosi cha Young Africans
kimekua kikiendelea na mazoezi kila siku tangu tangu baada ya mchezo wa
jumapili, ambapo kocha mkuu Marcio Maximo amekua akiwanoa vijana wake
kuhakikisha wanakua fit kwa mchezo huo wa jumamosi.
Young
Africans chini ya mbrazil Marcio Maximo imepania kuhakaikisha safari
hii inavunja mwiko wa kukosa ushindi katika dimba la Jamhuri kwa
takribani miaka minne mfululizo, na maandalizi ya mchezo yanakwenda
vizuri kuhakikisha kikosi kinaibuka na pointi tatu muhimu.
Kocha
Mkuu Marcio Maximo mara baada ya mazoezi ya leo katika shule ya
Sekondari Loyola, amesema vijana wake wote fit kwa mchezo huo na kikosi
kinatarajia kuondoka asubuhi ili vijana waweze kupata muda mzuri wa
kupumzika.
Aidha Maximo
amesema anatambua Mtibwa Sugar wana kikosi kizuri ambacho kimekaa pamoja
kwa muda mrefu, baadhi ya wachezaji aliwahi kuwafundisha akiwa kocha wa
timu ya Taifa (Taifa Stars) ikiwa ni pamoja na kocha wao Mecky Mexime.
"Sisi
tumejiandaa kuhakikisha tunapata ushindi katika mchezo wa jumamosi,
natambua utakua ni mgumu sababu Mtibwa watakua nyumbani wakihitaji
pointi tatu muhimu lakini hata sisi tunakwenda Morogoro kuhakikisha
tunapata pointi tatu pia "alisema Maximo.
Kuhusu
maendeleo ya mchezaji Andrey Coutinho na Jerson Tegete wanaendelea
vizuri na mazoezi lakini daktari ameona wabakie jijini Dar es salaam
wakiendelea na programu nyingine chini ya usimamizi wa madaktari na
wataungana na kikosi kitakaporejea jijini kwa mazoezi ya pamoja.
Wachezaji wanaotarajia kusafiri kesho kuelekea Morogoro ni:
Makipa: Deo Munishi "Dida", Juma Kaseja na Ally Mustafa "Barthez"
Walinzi: Juma Abdul, Oscar Joshua, Rajab Zahir, Kelvin Yondani na Nadir Haroub "Cannavaro"
Viungo: Mbuyu Twite, Omega Seme, Hassan Dilunga, Nizar Khalfani, Haruna Niyonzima na Said Juma "Makapu"
Washambuliaji: Said Bahanuzi, Hussein Javu, Hamis Kizza, Geilson Santos "Jaja", Saimon Msuva na Mrisho Ngasa
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni