SIMBA italazimika kumlipa beki Donald Mosoti jumla ya Sh48.5 milioni baada ya kuvunja mkataba wake uliobakiza mwaka mmoja na nusu.
Kwa kuvunja mkataba tu, Mosoti anaidai Simba Dola
29,250 (Sh47.5Milioni) na kiasi kingine anachodai ni Dola 600 (Sh
975,684) zilizobaki katika usajili ambapo jumla yake ni Sh 48.5 milioni.
Pia Mosoti anamlipa Mwanasheria wake dola 2,000 (Sh3.25 milioni) kwa
ajili ya kusimamia kesi hiyo.
Tayari Mwanasheria wa Mosoti, Felix Majani, ambaye
pia ni mmoja wa wanasheria wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa),
amefungua kesi katika shirikisho hilo kuwashitaki Simba kwa kukiuka
makubaliano ya mkataba na mteja wake.
Kabla ya kufungua kesi hiyo, Majani aliiandikia
barua Simba akiitaka kukaa mezani ili kumaliza suala hilo, barua ambazo
Rais wa Simba Evans Aveva amekiri kuzipokea, hata hivyo hawakuzifanyia
kazi.
Baada ya kuona ukimya ukiendelea kutawala,
Mwanasheria huyo ambaye aliwapa siku tatu Simba na kuwataka kumrudisha
mchezaji huyo kambini na kupeleka jina lake Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), ndipo alipoamua kufungua kesi hiyo.
“Niliyofanyiwa Simba ni unyama, ndio maana nimeona
Mwanasheria wangu asimamie mwenyewe labda litakuwa fundisho hata kwa
viongozi wengine,” alisema Mosoti.
“Sasa hivi wananiambia nitakuwa nafanya mazoezi na timu jambo ambalo halipo katika makubaliano ya mkataba wetu.”
Rais wa Simba, Evans Aveva alisema: “Ni kweli tumepata barua hizo tunazishughulikia.”
Moto umewaka katika kambi ya timu hiyo ikidaiwa
Aveva amekasirishwa na kitendo cha baadhi ya viongozi kumuondoa Mosoti
bila maelekezo yake.
MWANASPOTI
MWANASPOTI
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni