Wakati aliyekuwa kocha mkuu wa Azam FC, Stewart Hall akishangazwa na kiwango kidogo cha timu hiyo katika mchezo wao wa juzi wa Ngao ya Hisani, kiungo wa Taifa Stars, Frank Domayo amekiri kuzidiwa uwezo na Yanga.
Hall, aliyekuwa miongoni mwa maelfu ya mashabiki
walioushuhudia Azam ikilala kwa mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Taifa,
alisema timu hiyo ilicheza chini ya kiwango katika mchezo huo hasa
kipindi cha pili ambacho waliruhusu mabao yote matatu.
“Azam iliyocheza leo (juzi) si ile ambayo
naifahamu. Imecheza vibaya na chini ya kiwango, kama uchezaji wao ndio
huu, inapaswa kufanya kazi ya ziada kwenye ligi,” alisema Hall kwa
kifupi na kuondoka uwanjani hapo.
Naye Domayo, ambaye amehamia Azam akitokea Yanga,
alisema timu yake ya zamani iliwazidi mbinu hasa kipindi cha pili na
kujikuta wakikubali kipigo hicho.
“Tulizidiwa mbinu hasa kipindi cha pili, wenzetu
walirudi vizuri na kucheza kwa kushambulia zaidi tofauti na sisi ambao
baadhi ya wachezaji walichoka kipindi cha pili,” alisema Domayo ambaye
hakucheza mchezo huo kutokana na kuwa majeruhi.
Wakati huohuo, kocha msaidizi wa Azam, Kally
Ongala amesema walifungwa kimchezo na hawana sababu ya kuchukuliana
hatua kwa matokeo waliyopata juzi.
“Ni bora kufungwa leo kuliko kesho. Hii ni
changamoto kwetu kabla ya ligi. Upungufu umeonekana na utafanyiwa kazi.
Si kama hatuna wachezaji wazuri, bali tumefungwa kimchezo, hiyo hatuna
haja ya ‘kuchinjana’ kwa matokeo haya,” alisema kocha huyo.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni