KIKOSI cha Simba kimewasili jioni ya leo visiwani
Zanzibar na kesho kinaanza programu ya mwisho ya maandalizi ya kujiwinda na ligi
kuu soka Tanzania bara inayotarajia kuanza kushika kasi septemba 20 mwaka huu.
Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’
amesema Zanzibar ni sehemu tulivu na rafiki kwa Simba, hivyo kocha Patrick
Phiri atatulia huko kabla ya kurejea jumamosi kujiandaa na mchezo wa jumapili
(septemba 21 mwaka huu) uwanja wa Taifa, Dar es salaam dhidi ya Coastal Union.
Ijumaa ya wiki iliyopita, Simba walifungwa 1-0 na
URA ya Uganda katika mechi ya kimataifa ya kirafiki uwanja wa Taifa na jumamosi
walikuwa na mechi na Ndanda fc uwanja wa Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara.
Mechi hiyo ambayo ilikuwa ya mwisho kwa kocha Phiri kupima uwezo wa kikosi chake ilimalizika kwa
suluhu pacha ya bila kufungana.
Kabla ya mechi hiyo, septemba 6 mwaka huu,Simba walishinda mabao 3-0 dhidi ya Gor Mahia ya Kenya katika mechi ya kwanza ya kimataifa ya kirafiki tangu kocha Phiri arejee msimbazi.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni