LOGO

 
MWANASOKA Bora wa Dunia na ulaya, Mreno Cristiano Ronaldo amefunguka nakusema kwamba Manchester United ni klabu ambayo ipo moyoni mwake na anatamani siku moja arudi kucheza kucheza tena kwenye timu hiyo yenye maskani yake kwenye uwanja wa Old Trafford.
Mchezaji huyo aliejiunga na Real Madrid mwaka 2009 akitokea Manchester United kwa ada ya iliyovunja Rekodi ya Dunia ya paund milion 80 akitokea Manchester United na ameweka wazi "NaipendaI Manchester," na kuongeza;
"Kila mmoja anajua hilo — nimesema hivyo mara nyingi. Manchester ipo moyoni mwangu. Nimeacha marafi wengi huko, mashabiki wanavutia sana na ninatamani siku moja ningerudi,". 
Cristiano Ronaldo alijiunga na Manchester United mwaka 2003 akitokea Sporting Lisbon ya kwao ureno kwa ada ya paund milion12 akiwa kinda wa miaka 17 tu na kufanikiwa kushinda mataji mengi likiwemo la UEFA CHAMPIONS LEAGUE mwaka 2008.

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top