Meneja wa timu hiyo, Nico Nyagawa alisema juzi
kuwa Kiongera atakuwa anatumia jezi hiyo lakini mambo yakawa tofauti
baada ya mshambuliaji huyo kugoma.
Kiongera aliomba apewe jezi namba 29, lakini pia ilikuwa ngumu kuipata kwani tayari namba hiyo alipewa beki Adam Miraji.
Akizungumza na gazeti hili juzi, Kiongera alisema
namba anazopenda kuzitumia ni 5 na 29, lakini zote zinatumiwa na
wachezaji wengine, ambapo viongozi wake wamedai kumpa namba 12, lakini
namba hiyo ameikataa.
“Mosoti bado yupo kwenye timu, wananipaje namba
anayovaa yeye, siwezi kuvaa namba hiyo, awali walinipa namba 29 ambayo
pia naipenda, lakini nimekuta wamempa mchezaji mwingine na
wananilazimisha kuchukua namba 12 ambayo siipendi,” alisema Kiongera.
Mchezaji huyo alijiunga na kambi hiyo Jumatatu na
kuanza rasmi mazoezi yake Jumanne, ambapo kocha Patrick Phiri alisema
atampa mazoezi maalumu kwa muda wa wiki moja ili awe sawa na wenzake
walioanza maandalizi muda mrefu.
Phiri alisema Kiongera atakuwa anafanya mazoezi ya
ufukweni na uwanjani, mazoezi ambayo mshambuliaji huyo amelalamika kuwa
ni magumu.
“Nimepewa mazoezi magumu lakini yananijenga kuwa
‘fiti, unajua sijafanya mazoezi na wenzangu, nitahakikisha nafanya kwa
bidii ili niwe sawa nao,” alisema.Wakati huo huo, usajili wa beki
Shaffih Hassan umekwama na kuifanya Simba kumpoteza beki huyo katika
safu yake ya ulinzi.
Hassan alijiunga na Wekundu wa Msimbazii mara baada ya kikosi hicho kutua Zanzibar na kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya KMKM.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni