KOCHA mpya wa Simba, Patrick Phiri, na Mchezaji mpya wa Simba, Emmanuel Okwi, Jioni hii wataonekana kwa mara ya kwanza Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam wakati Simba inacheza Mechi ya Kirafiki na Mabingwa wa Kenya Gor Mahia.
Okwi amechukuliwa na Simba kutoka Yanga na kuzua utata mkubwa ambao sasa umetua TFF hasa kwa vile Yanga wanadai Mchezaji huyo amekiuka Mkataba wake na Yanga wa Miaka miwili na Nusu.
Pamoja na Okwi, Simba pia itamtumia Mchezaji wao mpya kutoka KCB, Kenya Commercial Bank, Paul Kiongera na hii itakuwa Mechi yake ya pili kwa Simba baada ya kucheza ile waliyokung’utwa 3-0 na ZESCO ya Uganda hapo Agosti 9.
Baada ya kipigo hicho, Simba walipiga kambi huko Zanzibar na kucheza Mechi 3 za kujipima na kushinda zote.
Jumapili, kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, Yanga watacheza Mechi ya Kirafiki na Big Bullets ya Malawi ambayo zamani ilikuwa ikiitwa Bata Bullets.
Hili ni pambano safi la kujipima kwa Yanga ambao Wikiendi ijayo watafungua rasmi Msimu mpya wa 2014/15 kwa kucheza pambano la kufungua pazia kugombea Ngao ya Jamii dhidi ya Mabingwa wa Tanzania Bara Azam FC.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni