LOGO

Manchester United boss Louis van Gaal is set to hand debuts to Radamel Falcao (left) and Daley BlindManchester United bado wanasaka ushindi wao wa kwanza baada ya Mechi 3 za Ligi Kuu England na Leo hii wako kwao kuivaa Timu iliyopanda Daraja QPR huku wakitegemea kuwatumia Wachezaji wao 6 wapya kwa pamoja kwa mara ya kwanza.
 Joey Barton is a fitness doubt for QPR after picking up a hamstring injury
Ingawa wanakabiliwa na Majeruhi 9, Man United hii Leo inaweza kuwatumia wapya kina Angel Di Maria, Marco Rojo, Radamel Falcao, Luke Shaw, Anders Herrera na Daley Blind.
Lakini QPR, chini ya Mene mkongwe Harry Redknapp, wanatinga kweye Mechi hii wakitoka kwenye ushindi wa Bao 1-0 dhidi ya Sunderland.
Mvuto kwa Mechi hii ni kurudi Old Trafford kwa Rio Ferdinand ambae aliitumikia Man United kwa Miaka 12 na mwanzoni mwa Msimu kuhamia QPR baada ya Mkataba wake kumalizika na kutoongezwa.
Hali za Wachezaji:
Man United wana Listi ndufu wa Wachezaji Majeruhi ambao ni Marouane Fellaini, Michael Carrick, Chris Smalling, Ashley Young, Sam Johnstone, Jesse Lingard, James Wilson, Reece James na Phil Jones.
QPR itamkosa Aleandro Faurlin lakini inaweza kuwatumia Wachezaji wapya wao Niko Kranjcar na Sandro.
Mara ya mwisho kukutana
Ni Februari 2013 wakati Rafael na Ryan Giggs, akiichezea Man Unite Mechi yake ya 999, walifunga Bao huko Loftus Road na kuipa ushindi wa Bao 2-0.
WAAMUZI
Refa atakuwa ni Phil Dowd akisaidiwa na Peter Kirkup na Scott Ledger huku Andre Marriner akiwa Mwamuzi wa Akiba.

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top