Leo klabu ya Dar Young African Yanga inajitupa uwanjani kumenyana na Chipukizi FC ya Zanzibar kwenye mechi ya kirafiki.
Hii itakuwa mechi ya kwanza kwa kocha mpya wa Yanga Mbrazil Marcio Maximo tangia ajiunge na Yanga akichukua nafasi ya
Mholanzi, Hans Van der Pluijm,
anatarajia kuwatumia wachezaji wote wa kikosi cha kwanza na cha pili ili kuona
namna walivyopokea mafunzo yake yaliyofanyika kwa muda mrefu uwanja wa shule ya
Sekondari, Loyola, iliyopo Mabibo jijini Dar es salaam.
Ingawa mechi hii itakayoanza majira
ya saa 10:00 jioni uwanja wa Gombani, Kisiwani Pemba ni ya kirafiki, lakini ina
umuhimu mkubwa kwa Maximo kwasababu anahitaji kuwaaminisha mashabiki wa Yanga
wenye imani kubwa na mwalimu huyu wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania,
‘Taifa Stars’ (2006-2010).
Viingilio katika mechi hiyo ni
shilingi elfu tatu (3,000/=) kwa VIP na elfu mbili (2,000/=)
majukwaa ya kawaida.
Mashabiki wa Yanga waliopo Pemba na
Zanzibar wanatarajiwa kufurika Gombani kuwaona vijana wa Yanga, hususani
Wabrazil wawili, Gleilson Santos Santana ‘Jaja’ na Andrey Coutinho ambao kwa
mara ya kwanza watacheza mechi ya kirafiki tangu wasajiliwe majira haya ya
kiangazi.
Kocha mkuuu Marcio Maximo na kikosi
chake wamefikia katika hoteli ya kitalii ya Pemba Misali iliyopo eneo la Wesha
na watajifua kwa takribani siku 10 kabla ya kurejea jijini Dar es salaam
mwishoni mwa mwezi huu.
Kulingana na program ya bench la
Ufundi kisiwani Pemba, Young Africans inatarajia kucheza michezo mitatu ya
kirafiki na timu za kutoka Visiwa vya Pemba na Unguja na baadaye kurejea Dar es
salaam kwa michezo miwili ya kimataifa kabla ya kucheza mchezo wa Ngao ya
Hisani septemba 13, 2014.
Wachezaji waliopo Pemba Walinda Mlango
Juma Kaseja, Ally Mustafa “Barthez” na Deogratias Munish “Dida”, Walinzi wa
Pembeni, Juma Abdul, Salum Telea, Oscar Joshua, Edwad Charles na Amos Abel
Walinzi wa Kati ni Kelvin Yondani,
Nadir Haroub “Cannavaro”, Rajab Zahir na Pato Ngonyani.
Viungo: Mbuyu Twite, Said Juma
“Makapu”, Omega Seme, Hassan Dilunga, Haruna Niyonzima na Hamis Thabit.
Viungo wa Pembeni: Saimon Msuva,
Mrisho Ngasa, Nizar Khalfani na Andrey Coutinho.
Washambuliaji: Geilson Santos
“Jaja”, Said Bahanuzi, Jerson Tegete, Hamis Kizza na Hussein Javu
Benchi la Ufundi walioko Kisiwani
Pemba ni:
Kocha Mkuu : Marcio Maximo
Kocha wasaidizi Leonado Neiva,
Salvatory Edward
Kocha wa Makipa: Juma
Pondamali
Daktari wa timu: Dr Suphian
Juma
Meneja wa timu: Hafidh Saleh
Mchua Misuli: Jaco Onyango
Mtunza Vifaa: Mahmod Omar
“Mpogolo”
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni