Kocha wa Yanga ya Dar es Salaam Marcio Maximo amesema kikosi chake kinaanza kupata kasi ambayo
anaitaka.
Hata hivyo amesisitiza bado anahitaji mechi za kirafiki ili kujipanga
vizuri zaidi.
“Mechi za kirafiki si kwa ajili ya pointi kwa kuwa hii si ligi, lakini
ni muhimu kwa maandalizi na kuangalia nini tumefanya kwenye maandalizi kabla ya
ligi,” alisema.
Tayari uongozi wa Yanga unalifanyia kazi suala la mechi za kirafiki
alizoomba kocha huyo ili kuweka kiwango chake vizuri kabla ya kuanza ligi.
Yanga ilikuwa Pemba na baadaye Unguja ambako ilicheza mechi za kirafiki
na kushinda zote.
Lakini bado Mbrazili huyo anataka mechi nyingine jijini Dar es Salaam
kujiweka sawa zaidi.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni