Rais wa klabu ya Yanga, Yusuph Manji
amesema kuwa klabu yake itawasilisha orodha ya wachezaji sita wa kigeni badala
ya watano wanaotakiwa kwa mujibu wa kanuni za usajili.
Akizungumza na vyombo vya habari
siku ya leo, Manji amesema kuwa majina hayo yataambatana na jina la
mshambulizi, Emmanuel Okwi ambaye jana klabu ya Simba SC ilitangaza kumsaini
kwa mkataba wa muda usijulikana.
Mbuyu Twite na Haruna Niyonzima
kutoka nchini Rwanda, Andrey Coutinho na Geilson Santos ‘ Jaja’ kutoka nchini
Brazil na Hamis Kizza ni majina mengine matano ambayo yatapelekwa kwa
shirikisho la soka nchini TFF, siku ya kesho.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni