LOGO

 

BAO 2 ndani ya Dakika 3 za kwanza ziliwapa Chelsea mwanzo mzuri Ugenini huko Goodison na Chelsea wakamaliza Mechi hii kwa ushindi wa Bao 6-3.
Bao hizo za mapema za Chelsea, zenye utata wa Ofsaidi, zilifungwa na Diego Costa na Ivanovic.
Everton walipata Bao lao la kwanza katika Dakia ya 45 kupitia Mirallas
.
Hadi Mapumziko Chelsea 2 Everton 1.
Kipindi cha Pili, Chelsea walipiga Bao la 3 mfungaji akiwa Coleman, alirjifunga mwenyewe, na Naismith kuipa Everton Dakika 2 baadae lakini Chelsea wakapiga Bao la Nne kupitia Matic na Dakika 2 baadae Mchezaji mpya wa Everton, Samuel Eto’o akaipigia Everton Bao la 3.
Huku Gemu ikiwa 4-3, Ramires akaipa Chelsea Bao la 5 katika Dakika ya 76 na Diego Costa akapiga Bao la 6 kuikata maini Everton.

VIKOSI:
Everton: Howard, Coleman, Jagielka, Distin, Baines, McCarthy, Barry, Mirallas, Naismith, McGeady, Lukaku.
Subs: Robles, Gibson, Eto’o, Besic, Osman, Stones, Alcaraz

Chelsea: Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Ramires, Matic, Willian, Fabregas, Hazard, Costa.
Subs: Cech, Luis, Zouma, Drogba, Mikel, Schurrle, Salah

Refa: Jon Moss

Everton 3
-Mirallas 45
-Naismith 69
-Eto'o 76
Chelsea 6
-Diego Costa 1 & 90
-Ivanovic 3
-Coleman 67 [Kajifunga mwenyewe]
-Matic 74
-Ramires 77

Kesho Jumapili zipo Mechi mbili za Ligi Kuu England kati ya Aston Villa na Hull City na kufuatia ile ya Leicester v Arsenal

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top