LOGO

Klabu ya Atletico Madrid ya spain imetwaa kombe la Super copa maarufu kwa ufunguzi wa ligi mpya nchini spain kwa kuwalaza mahasimu Real Madrid kwa goli 1-0 goli likifungwa na mshambuliaji wao mpya Mario Mandzukic dakika ya 2 baada ya kupokea pasi ya mchezaji mwingine mpya Antoine Griezmann katika mchezo uliochezwa kwenye dimba la Vicente Calderon jijini Madrid.
 
Jumla inakuwa ni goali 2-1 ambapo mchezo wa kwanza walitoka sare ya goli1-1 kwenye dimba la Santiago Bernabeu
Katika mchezo huo madrid waliwakosa wachezaji wake nyota Muargentina Angel Di Maria na Mjerumani Sami Khedira ambao wanahusiishwa kuhama klabuni hapo na kutimkia Manchester United kwa Di Maria na Bayern Munich kwa Khedira.
 
Katika dakika ya 90 mchezaji Luka Modric wa Real Madrid akitolewa kwa nyekundu baada ya kupata kadi mbili za njano huku kocha wa Atletico Madrid nae akitolewa nje kwa kadi nyekundu.
 
VIKOSI VILIKUWA KAMA IFUATAVYO 

Atletico Madrid
  Moya; Juanfran, Godín, Miranda, Siqueira; Tiago, Gabi; Koke, Raul García, Griezmann (Jiminez 73); Mandzukic
Subs: Oblak, Suarez, Rodriguez, Ansaldi, Niguez, Gimenez
  
 Goal: Mandzukic 2

  •  Real Madrid 
     Casillas; Carvajal, Varane, Ramos, Coentrao (Marcelo 70); Modric, Kroos (Ronaldo 45), Xabi Alonso; James (Isco 65), Benzema, Bal
      Subs: Navas, Pepe, Arbeloa, Illarra 
     
    Referee: Fernandez Borbalan (Spanish) 

  • 0 comments Blogger 0 Facebook

    Chapisha Maoni

    ZILIZOSOMWA SANA

     
    TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
    Top