Aprili 26, mwaka huu katika kuadhimisha miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Stars iliyokuwa imeweka kambi ya mwezi mzima mjini Tukuyu, Mbeya kwa maamuzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ilianza na wachezaji watano wa maboresho wasiokuwa na uzoefu na kufungwa nyumbani Uwanja wa Taifa mabao 3-0 dhidi ya timu ya Taifa ya Burundi ‘Entamba Murugamba’.
Kikosi cha pili cha Stars ‘Taifa Stars Maboresho’ kimeleat huzuni tena katika siku ya furaha kwa Watanzania leo baada ya kupokea kichapo hicho.
Kikiongozwa na Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mholanzi Mart Nooij, Kikosi cha Taifa Stars Maboresho kilikuwa cha kwanza kupata bao dakika ya 11 kupitia kwa Yusuph Rashid kabla ya kuonesha udhaifu mkubwa katika safu ya kiungo na kuwaruhusu wageni kutawala mchezo na kurudisha bao kisha kuongeza la ushindi.
Alikuwa Fabrice Mimimahazwe aliyefunga bao la kwanza dakika ya 25 kutokana na udhaifu wa safu ya kiungo ya Stars Maboresho iliyoruhusu wageni wauchezea mpira watakavyo, utadhani Burundi walikuwa wenyeji wa mechi hiyo.
Bao la pili la Burundi U-23 limefungwa na Nassor Niyonkuru dakika ya 72 ya mchezo. Baada ya bao hilo, Stars Maboresho walijaribu kubadilisha matokeo lakini kipa Innocent Mbonihankuye alikuwa mwiba mkali.
Mechi hiyo iliandaliwa na TFF kwa ajili ya kusherehekea miaka 53 ya Uhuru wa Tanganyika. Kabla ya mechi hiyo Stars Maboresho waliweka kambi kwenye Machimbo ya Dhahabu, Bulyang’hulu mkoani Shinyanga.
Kikosi cha Stars kilikuwa: Aishi Manula, Miraj Adam, Gadriel Michael, Joramu Mgeveke/ Emmanuel Semwanda (dk 90), Andrew Vincent, Salum Mbonde, Rashid Yusuph/ Omar Njenje (dk 80), Hassan Banda, Atipele Green, Kelvin Friday/ Mohamed Abubakar (dk 70) na Hussein Moshi/ Ramadhani Shiza (dk 62
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni