LOGO


Uzembe wa mabeki wa klabu ya Yanga sc umesababisha timu hiyo kupoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya Simba SC katika mchezo wa kuwania kombe la nani mtani jembe kwenye mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo ulioandaliwa na Mdhamini mkuu wa Klabu hizo kongwe na zenye mashabiki wengi nchini Tanzania kampuni ya bia ya TBL kupiutia bia yao ya Kilimanjaro ulishuhudia Yanga kupoteza kwa mabao hayo ikiwa ni mara ya pili mfululizo kwani December mwaka jana Yanga ilipoteza tena kwa jumla ya magoli 3-1 dhidi ya Simba na kusababisha kufukuzwa kwa kocha mkuu Mholanzi Ernest Brands.

Alikuwa ni Awadhi Juma alieipatia Simba SC goli la kuongoza baada ya kuunganishwa mpira uliopigwa na Mganda Emmanuel Okwi katika dakika ya 30 baada mabeki wa Yanga kuzubaa na kushindwa kuokoa mpira mpira huo uliopigwa na Okwi na kufanya matokeo kusomeka Simba SC 1 Yanga SC 0 
Yanga SC walijitahidi kurudisha bao hilo kupitia kwa washambuliaji wao mpya kutoka mchini Algeria Kpah Sherman alieoneka na anaweza kukaa na mpira na kushambulia vizuri lakini akakosa ushirikiano mzuri kutoka kwa wenzanke lakini uimara wa mabeki wa Simba pamoja na kipa wao Ivo Mapunda ulisimama imara kuhakikisha Yanga wanashindwa kutia mpira katika kimia chao.

Katika dakika ya 42 ya mchezo huo Simba SC ilijipatia bao la pili kupitia kwa mshambuliaji wake Elias Maguri alieonganisha krosi safi ya Simon Ssrenkuma baada ya kupiga kichwa awali na kugonga mwamba ambapo mabeki wa Yanga walishindwa kuokoa tena hatari hiyo langoni mwao na Maguri kufunga bao la pili kiulaini hadi mapumziko Simba 2 Yanga 0.

Katika kipindi cha pili Yanga walionekana kutokuwa na mipango haswa katika safu yao ya Ushambuliaji kwa kukosa mabao kadhaa ya wazi pamoja na kupiga mipira isiyokuwa na madhara langoni kwa Simba
Timu zote zilifanya mabadiliko katika vikosi vyao ambapo Klabu ya Simba ilimtoa Juuko Murushid na kumuingiza nahodha Joseph Owino, Ramadhani Singano Messi alitoka na kuingia Said Ndemla huku Danny Ssrenkuma akiingia na kucheza dakika 6 za mchezo baada ya kutoka Elias Maguri kwa upande wa Yanga Danny Mrwanda aliingia kuchukua nafasi ya Mbrazil Andrei Coutinho, Emerson Roque alitoka na nafasi yake kuchukuliwa na Salum Telela huku Mrisho Ngasa akichukua nafasi ya Kpah Sherman hata hivyo mabadiliko hayo hayakuweza kubadilisha matokeo ya mchezo hadi dakika 90 zinaisha kwa Yanga kulala mabao 2-0.

Mchezo huo uliochezeshwa na Refa mwanamke kutoka mkoani Kagera aliweza kumudu kuchezesha kwa ustadi mkubwa kwa dakika zote. Emmanuel Okwi alieonekana kuwa Sumu kwa wakati wote katika lango ya Yanga kwa kutengeneza nafasi nyingi za kufunga na kuwanyanyasa muda wote wa mchezo

Mashabiki wa Yanga walianza kuondoka uwanjani mara baada ya bao la pili kuingia huku mashabiki mwa Simba waSimba wakishangilia na kubeba Jeneza lilio na nembo na Bendera ya Yanga.
Kwa ushindi huo Simba imezawadiwa kikombe na pesa taslimu shilingi milioni 92 ambapo miloni 10 wameshinda uwanjani na milioni 82 zingine walishinda kutokana mashabiki kupiga kura kwa timu yao huku Yanga ikilamba milioni 8 pekee kwa kura na pesa ya mshindi wa pili.

VIKOSI
YANGA:
Deo Dida, Abdul Juma/Hussein Javu dk 73, Oscar Joshua, Nadir Haroub, Kelvin Yondani, Mbuyu Twite/Hassani Dilunga dk 39, Haruna Niyonzima, Emerson Roque/Salum Telea dk 55, Simon Msumva, Kpah Sherman/Mrisho Ngassa dk 63, Andrei Coutinho/Danny Mrwanda dk 46

SIMBA:
Ivo Mapunda, Nassor Chollo, Mohammed Hussein/Issa Rashid dk 66, Hassan Isihaka, Juuko Murishid/Joseph Owino dk 47, Jonas Mkude, Ramadhani Singano/Said Ndemla dk 74, Awadhi Juma, Elias Maguri/ Dani Sserunkuma gk 84, Simon Sserunkuma/Shabani Kisiga dk 84, Emmanuel Okwi

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top