LOGO

https://kifltd.files.wordpress.com/2012/04/nyoso.jpg

Mlinzi wa kati Juma Nyosso amejiunga na kikosi cha Mbeya City Fc kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Akizungumza mara baada ya kuisaini mkataba  huo kwenye  ofisi za timu zilizopo jengo la Mkapa Hall jijini Mbeya,  Nyoso aliyewahi kucheza kwenye timu za Ashanti United, Simba na Coastal Union, alisema  amekubari kujiunga na City kwa mkataba wa mwaka mmoja kwa imani kuwa utatosha  kuushawishi uongozi wa timu kumpa mkataba mrefu zaidi mara baada ya huu wa sasa.

“City ni timu nzuri na imekuwa hivyo toka ilipoanzishwa miaka minne iliyopita, matokeo yaliyoo sasa ni sehemu ya soka ambayo timu yoyote inaweza kuyapata, nimekubari kujiunga na timu kwa  mkataba wa mwaka mmoja kwa sababu naamini uwezo wangu  uwanjani utawashawishi viongozi kunipa mkataba mrefu zaidi  pindi huu utakapo malizika na nina amini  hili

linawezekana kwa sababu nataka kukaa kwenye timu hii mpaka mpira wangu utakapoisha” alisema Nyosso
Akiendelea zaidi beki huyo aliyewahi pia kucheza  kwenye kikosi cha timu ya Taifa  ‘Taifa Stars’ alisema kuwa  mafanikio iliyopata Mbeya City msimu uliopita yamekuwa sababu kubwa ya yeye kukubari kujiunga na City huku akiamini kuwa amekuja kuongeza nguvu kwenye timu bora ili kuhakikisha mafanikio ya msimu uliopita yanafanikiwa tena.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa City Emmanuel Kimbe alimshukuru Nyosso kwa kukubari kujiunga na timu hii huku akiamini kuwa uzoefu alionao mchezaji huyo utasaidia kuimarisha safu ya ulinzi kwenye kikosi cha City.
“Tunamshukuru kukubari kujiunga nasi, imani yetu kubwa kwamba uzoefu alionao utasaidia kuimarisha safu yetu ya ulinzi, hasa ukizingatia matokeo tuliyopata katika michezo saba ya mwanzo wa Ligi hii” alisema Kimbe huku   kauli yake hiyo ikiungwa mkono na Kocha Mkuu Juma Mwambusi.
Kwa sasa Nyosso tayari yuko na kikosi cha City kilichosafiri kwenda mjini Songea  kwa ajiri ya michezo ya kirafiki.

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top