Viungo vya simba sc na yanga, Haruna Chanongo na Omega Seme wameenda kwa mkopo katika timu zilizo panda ligi kuu ya Tanzania bara, stand united na ndanda fc.
Usajili wa wachezaji hao wa wili ni miongoni mwa usajili uliokamilishwa jana, ambapo dirisha lake la usajili likitarajiwa kufungwa desemba 15 mwaka huu.
Stand united jana walikamilisha usajili wa wachezaji Haruna Chanongo kutoka simba sc, huku Ndanea wakifanikiwa kumnasa Omega Seme kutoka yanga sc kwa mkopo.
Nao Polisi Morogoro hawakuwa nyuma katika uzibaji wa pengo la Danny Mrwanda aliyejiunga na yanga kwa kumsajili kwa mkopo Said Bahanuzi kutokea yanga sc. Ruvushooting nao juzi walikamilisha usajili wa mshambuliaji wa zamani yanga na azam fc, Yahya Tumbo kutoka klabu ya Mtende rangers inayoshiriki ligi kuu ya Zanzibar.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni