Katibu
Mkuu wa Malindi Mohammed Masoud Rashid, amesema si Zimamoto wala Ashanti United yenye haki ya kumtumia au kumuuza
mwanasoka huyo.
Kwa hivyo, Malindi ameitahadharisha Simba kutokufanya kosa, na kama inamtaka beki huyo inalazimika kufanya mawasiliano na uongozi wa timu hiyo na kufuata taratibu za usajili.
Masoud alieleza kushangazwa na hatua ya Simba kudai kuwa wamemsajili mchezaji huyo kutoka Ashanti United, wakati klabu anapaswa kuhamishwa kutoka Malindi.
Katibu huyo alidai kuwa, Shafii ana mkataba wa miaka miwili klabu yake ambao bado haijamalizika, hivyo kitendo cha Ashanti United msimu uliopita kumsajili, hakikuwa halali.
Masoud alisema usajili huo ulifanywa kwa mabavu na Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) kwa kushirikiana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), na kusisitiza kuwa ni vyema Simba iwasiliane na uongozi wa Malindi yenye mkataba na mchezaji huyo.
"Tunaitahadharisha Simba kwamba Shafii ni mchezaji wetu na si wa Zimamoto wala Ashanti. Ssisi hatutaki ugomvi nao lakini kama hawakuja kumsajili kwetu tupo tayari kwenda popote kudai haki yetu," alisema Masoud.
Masoud alidai hiyo si mara ya kwanza Simba kuwatenda kwani walishawahi kumnyakua kijanja mchezaji wao Adeyoum Saleh, lakini wakawaachia kwa kuwa hapo mwanzo walikuwa na udugu mzuri.
"Aliposajiliwa Shafii Ashanti tulipeleka malalamiko ZFA, lakini wakaamua kutupuuza, hivyo tunaamini alisajiliwa kwa matakwa na maslahi ya viongozi wa ZFA na TFF kwa kutumia vyeo vyao," alidai.
Katibu huyo alifika mbali zaidi kwa kutamka wazi kwamba timu ya Zimamoto inahusika kwa kiasi kikubwa katika kumtorosha mchezaji huyo kwenda Ashanti, ili waweze kumsajili kirahisi.
"Katika hili TFF, ZFA, Zimamoto na Ashanti wote walihusika kumtorosha kwani tulipowasiliana na TFF kipindi hicho walitujibu kuwa hawawezi kulishughulikia suala hilo," aliongeza.
Akizungumzia kadhia hiyo, Raisi wa ZFA Ravia Idarous, ameishangaa Malindi, akidai kuwa wakati wa dirisha dogo msimu uliopita, mchezaji huyo alichezea Ashanti hadi mwisho wa ligi, lakini klabu hiyo ilikaa kimya.
Alisema ZFA ilimuidhinisha mchezaji huyo aliyekuwa huru kuichezea Ashanti baada ya timu hiyo kukamilisha taratibu zote za usajili, na kwamba hafahamu Malindi inatumia vigezo gani kudai Shafii ni mali yake.
Naye Katibu wa Zimamoto Ali Jongo akimshangaa Katibu wa Malindi inapata wapi jeuri ya kudai mchezaji huyo ni wao, na kuongeza kuwa hawana muda wa kulumbana, bali wanashughulikia mambo mengine yaliyopo mbele yao.

0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni