Timu ya soka ya Mbeya City kutoka Jijini Mbeya inayoshiriki ligi kuu ya Tanzania bara imeweka kambi nje ya mji kwa ajili ya kujiandaa na ligi hiyo msimu ujao itakayoanza kutimua vumbi september 20 mwaka huu.
Timu hiyo inayodhaminiwa Kampuni ya Bin Slum Tyre inaonekana kupania kufanya vizuri
zaidi msimu ujao kwa kujiandaa vizuri chini ya kocha wao Juma Mwambusi
“Tumeamua kuweka
kambi nje ya mji wa Mbeya kwa ajili ya kujiimarisha zaidi na mwalimu Juma
Mwambusi anaendelea na maandalizi.
“Lengo ni kucheza
michuano ya kimataifa ukizingatia Mbeya City ni kati ya timu zinazotupiwa macho
na wengi.
“Hivyo lazima
kujiandaa vilivyo na tunataka kufanya vizuri ingawa tunajua si kazi lahisi,”
alisema Dismas.
Mbeya City ilimaliza
msimu uliopita ikiwa katika nafasi ya tatu nyuma ya mabingwa Azam FC na Yanga
walioshika nafasi ya pili.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni