MAKUNDI
MATOKEO
Jumanne Septemba 16
KUNDI A
Juvsentus 2 Malmö FF 0
Olympiakos 3 Atlético Madrid 2
KUNDI B
Liverpool 2 Ludogorets Razgrad 1
Real Madrid 5 FC Basel 1
KUNDI C
Benfica 0 Zenit St Petersburg 2
Monaco 1 Bayer 04 Levserkusen 0
KUNDI D
Borussia Dortmund 2 Arsenal 0
Galatasaray 1 RSC Anderlecht 1
REAL MADRID 5 FC BASEL 1
MABINGWA WATETEZI wa Ulaya, Real Madrid, wakiwa kwao Santiago Bernabeu wameanza utetezi wa Taji lao vyema kwa kuitandika FC Basel ya Uswisi Bao 5-1 katika Mechi ya kwanza ya Kundi B la UEFA CHAMPIONZ LIGI. Real waliongoza 4-1 kufikia Haftaimu kwa Bao za Suchy aliejifunga mwenyewe Dakika ya 14, Gareth Bale, 30, Ronaldo, 31, na James Rodriguez, 36 huku FC Basel wakifunga Bao lao Dakika ya 38 kupitia Gonzalez.
Kipindi cha Pili, Dakika ya 79, Karim Benzema alifunga Bao la 5 kwa Mabingwa wa Ulaya Real Madrid.
Hadi mwisho Real 5 FC Basel 1.
VIKOSI:
REAL MADRID: 01 Casillas, 12 Marcelo, 18 Nacho, 04 Ramos, 03 Pepe, 11 Bale, 19 Modric, 08 Kroos, 10 Rodríguez, 07 Ronaldo, 09 Benzema
Akiba: 02 Varane, 05 Fábio Coentrão, 13 Navas, 14 Hernández, 17 Arbeloa, 23 Isco, 24 Illarramendi
FC BASEL: 01 Vaclik, 16 Schär, 06 Samuel, 17 Suchy, 20 Frei, 33 Elneny, 19 Safari, 34 Xhaka, 09 Streller, 25 González, 07 Zuffi
Akiba: 10 Delgado, 11 Gashi, 14 Kakitani, 18 Vailati, 27 Aliji, 36 Embolo, 39 Callà
REFA: Damir Skomina (Slovenia)
LIVERPOOL 2 LUDOGORETS RAZGRAD 1
Penati ya Dakika za Majeruhi ya Steven Gerrard iliwapa Liverpool ushindi wa Bao 2-1 walipocheza na Ludogorets Razgrad ya Bulgaria katika Mechi ya kwanza ya Kundi B la UEFA CHAMPIONZ LIGI Uwanjani Anfield.
Straika mpya, Mario Balotelli, aliwapa Liverpool uongozii wa Bao 1-0 katika Dakika ya 82, hilo likiwa ni Bao la kwanza kwa Balotelli kwa Klabu yake, lakini Dakika ya 90 Wachezaji wawili waliotokea Benchi, Younes Hamza na Dani Abalo walishirikiana vyema na Abalo kusawazisha.
Penati iliyozaa Bao la ushindi ilitokea baada Kipa Borjan kudaiwa kumwangusha Borini
Hadi mwisho Liverpool 2 Ludogorets Razgrad 1.
VIKOSI:
LIVERPOOL: 22 Mignolet, 18 Moreno, 19 Manquillo, 06 Lovren, 17 Sakho, 10 Coutinho, 08 Gerrard, 31 Sterling, 20 Lallana, 14 Henderson, 45 Balotelli
Akiba: 01 Jones, 03 Jose Enrique, 04 K Touré, 09 Lambert, 21 Lucas, 29 Borini, 30 Fernández Saez
LUDOGORETS RAZGRAD: 26 Borjan, 15 Aleksandrov, 25 Minev, 27 Moti, 80 Paula Junior, 18 Dyakov, 93 Misidjan, 12 Andrianantenaina, 84 Nascimento da Costa, 07 Aleksandrov, 09 Bezjak
Akiba: 01 Gospodinov, 08 Gomes Fonseca, 16 Angulo, 17 Abalo Paulos, 23 Zlatinski, 88 Cristaldo Farias, 99 Younes
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni