LOUIS van Gaal amepata ushindi wa kwanza
tangu aanze kuiongoza Manchester United katika michuano ya ligi kuu
England kufuatia ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya QPR.
Mabao ya United katika mechi hiyo
iliyopigwa uwanja wa Old Trafford yamefungwa na Juan Mata, Wayne, Ander
Herrera na Angel di Maria.
Di Maria aliyeliliwa na Cristiano
Ronaldo baada ya kuondoka Real Madrid majira ya kiangazi mwaka huu
alifunga bao lake la kuongoza kwa njia ya mpira wa adhabu ndogo.
Herrera alifunga bao la tatu, wakati Wayne Rooney alifunga la tatu na Mhispania, Juan Mata alihitimisha karamu ya mabao.
Radamel Falcao alianzia benchi katika
mechi ya leo, wakati Daley Blind na Marcos Rojo walianza katika mechi
yao ya kwanza United.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni