MWALIKO WA KUSHIRIKI MASHINDANO YA NGUMI YA TAIFA
YATAKAYOSHIRIKISHA MIKOA YOTE YA TANZANIA BARA ,
DAR ES SALAAM 08-14/10/2014
Tafadhari sana husika na mada hapo juu,
Shirikisho
la ngumi Tanzania (BFT) limeandaa mashindano ya ngumi ya Taifa,
yatakayofanyika kuanzia tarehe 08-14/10/2014 jijini Dar es salaam. Siku
ya kumbukumbu ya kifo cha baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
Mashindano
yatashindanisha mabondia kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na timu
kutoka katika vyombo vya ulinzi na usalaama kama wanachama wa BFT.
Lengo la
mashindano ni kupata timu mpya ya taifa kwa maandalizi ya mashindano ya
kanda ya tatu ya Afrika 2015, Michezo ya Afrika 2015,Ubingwa wa dunia
2015, Michezo ya Olimpiki 2016 na mashindano mbalimbali tutakayoalikwa
ndani na nje ya Tanzania.
Pia
Mashindano hayo yatahusisha mabondia vijana (youth), wakubwa (senior),
na wanawake (women) kwa ratiba maalum ambayo itapangwa na wataalam wa
BFT.
Mpangilio na taratibu za kuweza kushiriki mashindano utakuwa kama ifuatavyo:-
· 29/09/2014: Mwisho wa kutuma majina ya washiriki wote katika
ofisi za BFT
· 07/10/2014: Timu zote kuwasili Dar es salaam
· 08/10/2014: Kupima uzito na afya na ufunguzi wa mashindano
· 09-10/10/2014: Mashindano kuendelea hatua ya mtoano
· 11-12/10/2014: Mashindano kuendelea Hatua ya nusu fainali
· 13/10/2014: Mashindano kuendelea hatua ya nusu fainali
· 14/10/2014: Mashindano kuendelea hatua ya fainali
· 15/10/2014: Timu zote kuondoka.
Kila
bondia atatakiwa kuja na kitabu cha kumbukumbu ya mashindano
(competition record book) na mavazi yake nadhifu ya kuchezea ngumi
ulingoni yanayokubalika katika sheria za mavazi za AIBA pamoja na mouth
guard.
Sheria na kanuni za chama cha ngumi cha dunia ( AIBA ) ndizo zitakazotumika wakati wote wa mashindano
Aidha
kila timu itatakiwa kujilipia nauli ya kuja na kurudi na malazi wakati
wote wa mashindano na BFT tutahusika na chakula kwa timu zote za kutoka
nje ya Dar es salaam, huduma za matibabu wakati wa mashindano pamoja na
masuala yote ya kiufundi.
Pia BFT itatoa vyeti kwa washiriki wote na medali kwa washindi.
Ada ya ushiriki wa kila timu ni Tsh. 50,000/= na italipwa sambamba na kuthibisha ushiriki kabla ya tarehe 29/09/2014.
NB:tunasisitiza
mwisho wa kutuma majina kwa washiriki wote na tarehe 29/09/2014 na
katika kutuma zingatia kuainisha jinsia, umri na kundi atakaloshiriki
yaani vijana ,wakubwa au wanawake na hakuna timu itakayoruhusiwa
kushiriki kama haitathibitisha kushiriki kwa wakati uliopapangwa ikiwa
pamoja na kulipa ada.
Nawatakia maandalizi mazuri
Makore mashaga
KATIBU MKUU
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni