Manchester United wakicheza Ugenini huko Turf Moor na Burnley, Timu
iliyopanda Daraja Msimu huu, wametoka Sare ya 0-0 na hii ni Mechi yao ya
3 ya Ligi Kuu England kwa Msimu mpya bila ushindi.
Kipindi cha Kwanza kilikuwa cha mashambulizi ya huku na huku na
Burnley wangeweza kupata Bao pale pasi ya nyuma ya Jonny Evans kwa Kipa
wake David De Gea kuwa fupi na kunaswa na Jutkiewicz lakini Kipa De Gea
akaokoa.
Man United wangeweza kupata Bao kwenye Kipindi hicho cha Kwanza baada
ya mchezo safi wa Mchezaji mpya Angel Di Maria, akiichezea Mechi yake
ya kwanza kabisa Man United, kumfungulia njia Robin van Persie ambae
shuti lake liliokolewa na Kipa Heaton.
Refa Chris Foy aliwanyima Penati ya wazi Man United wakati Beki wa
Burnley Trippier alipomsukuma Ashley Young na kumwangusha ndani ya
Boksi.
Kipindi cha Pili Man United walitawala na kunyimwa tena Penati wakati
Young alipopiga Shuti na Barnes kuunawa lakini kwa mara ya Pili Refa
Chris Foy alipeta.
Hadi mwisho, Burnley 0 Man United 0.
VIKOSI:
Burnley: Heaton, Trippier, Shackell, Duff, Mee, Arfield, Marney, Jones, Taylor, Jutkiewicz, Ings.
Akiba: Wallace, Sordell, Reid, Gilks, Ward, Long, Barnes.
Manchester United: De Gea, Jones, Evans, Blackett, Valencia, Fletcher, Di Maria, Young, Mata, van Persie, Rooney.
Akiba: Januzaj, Hernandez, Welbeck, Anderson, Michael Keane, Amos, James.
Refa: Chris Foy
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
ZILIZOSOMWA SANA
-
MICHUANO ya kombe la Mapinduzi 2015 iliyoanza kutimua vumbi jana inatarajia kuendelea tena leo kwa mitanange mitatu kupig...
-
Nahodha wa Liverpool Steven Gerrard ametangaza kuwa ataondoka Liverpool mwishoni mwa msimu huu baada ya kudumu liverpool kwa kipindi cha mi...
-
Siku kadhaa baada ya Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), kuifungia Kampuni ya Lino International kuendesha mashindano ya Miss Tanzani...
-
LIGI KUU ENGLAND Wikiendi hii inaanza kwa Mechi ya Jumamosi ya mapema kabisa huko...
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni