Klabu ya Manchester City imeibuka na ushindi wa magoli 3-1 dhidi Liverpool kwenye mchezo wa ligi kuu nchini England katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Etihadi.
Alikuwa ni Stevan Jovetic aliefungua karamu ya magoli kwa manchester City kwa kufunga bao safi katika dakika ya 41 ya mchezo na kufanya Manchester City kuongoza goli 1 hadi mapumziko.
Kipindi kilianza kwa tahadhari kubwa huku majogoo wa liverpool wakikata kusawazisha goli hilo lakini dakika ya 55 tu ya mchezo Jovetic tena akawainua vitini mashabiki wa Manchester City kwa kuongeza goli la pili na kufanya matokea kuwa 2-0.
Mchezaji alieingia kipindi cha pili kwa kwa kupokezana na Dzeko, Sergio Aguero akawahakikishia Manchester City ushindi kwa kufunga goli la 3 katika dakika ya 68 ikiwa ni sekunde 23 tangia aingie uwanjani.
Mchezaji mpya wa Liverpool Rickie Lambart aliifungia liverpool goli la kufutia machozi ikiwa pia ni goli lake la kwanza tangu ajiunge na Liverpool akitokea Southampton katika dakika ya 83 ya mchezo na kufanya matokeo kuwa 3-1 hadi dakika 90 za mchezo huo zinakamilika.
Mchezaji mpya wa Liverpool Mario Balloteli akiwa jukwaani akiangalia mchezo akiwa ni muda mfupi baada ya kutambulishwa rasmi kuichezea Liverpool.
Man City: Hart, Zabaleta, Kompany, Demichelis, Clichy, Nasri, Toure, Fernando, Silva, Jovetic, Dzeko.
Subs: Sagna, Milner, Kolarov, Caballero, Jesus Navas, Aguero, Fernandinho.
Goals: Jovetic 41, 55, Aguero 68
Liverpool: Mignolet, Johnson, Skrtel, Lovren, Moreno, Henderson, Gerrard, Allen, Coutinho, Sturridge, Sterling.
Subs: Brad Jones, Toure, Lambert, Sakho, Manquillo, Can, Markovic.
Goals: Lambert 83
Referee: Michael Oliver (Northumberland)
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni