Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Cameroon na klabu ya Everton Samuel Etoo,33 ametangaza rasmi kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Cameroon baada ya kuitumikia kwa kipindi cha miaka 17 hii imekuja muda mfupi baada ya Etoo kupokonywa cheo cha unahodha wa Cameroon na Chama cha soka cha nchi hiyo na Nafasi kuchukuliwa na Stephane Mbia kama nahodha mpya wa Cameroon.
Mbia, mwenye Miaka 28, ni Kiungo Mkabaji wa Sevilla akichezea Klabu hiyo ya Spain kwa Mkopo kutoka Klabu ya England Queen Park Rogers.
Mbia alianza kuichezea Cameroon Mwaka 2005 na ameshacheza Mechi 49 na kufunga Bao 3.
Sambamba na uteuzi huo wa Mbia, Wizara ya Michezo ya Cameroon pia iliwatangaza Straika wa Schalke 04 ya Germany, Eric Maxim Choupo-Moting, na Mchezaji wa FC Porto ya Ureno, Vincent Aboubakar, kuwa ni Makamu wa Nahodha Mbia.
Eto’o, ambae Juzi amesaini kuichezea Everton, ameichezea Cameroon kwa Miaka 17 akicheza Mechi 118 na kuweka Rekodi ya kufunga Bao 56 tangu alipoanza kucheza kama Kijana wa Miaka 15 Mwaka 1997.
Akitangaza kustaafu kwake, Eto’o amesema: “Napenda kujulisha kwamba sasa imestaafu kucheza Mechi za Kimataifa. Napenda kuwashkuru Waafrika wote na Mashabiki wangu Dunia nzima kwa upendo na sapoti isiyoyumba. Pokeeni shukrani zangu za dhati kabisa.”
Eto'o alicheza Fainali 4 za Kombe la Dunia, Fainali mbili za Mataifa ya Afrika, Mwaka 2000 na 2002, na alikuwa kwenye Timu ya Cameroon iliyotwaa Ubingwa wa Michezo ya Olimpiki Mwaka 2000.
0 comments Blogger 0 Facebook
Chapisha Maoni