LOGO


Mshambuliaji Fernando Torres wa chelsea amekubali kuondoka chelsea na kujiunga na AC Milan ya Italia
Mchezaji huyo wa Hispania aliedumu chelsea kwa miaka mitatu na nusu  anakwenda kuziba pengo la Mario Balotelli ambaye Milan imemuuza kwa Pauni Milioni 16 Mtaliano huyo Liverpool.
Wakala wa Torres alifanya mazungumzo na Milan Alhamisi asubuhi na mshambuliaji huyo amekubali kujiunga na vigogo hao wa Italia kwa miaka miwili.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 anahamia San Siro kwa mkopo wa miaka miwili.
Torres aliyetua Stamford Bridge kwa dau la Pauni Milioni 50 alikuwa amebakiza miaka miwili katika mkataba wake wa Pauni 150,000 kwa wiki Stamford Bridge na inaaminika wawakilishi wake walipatana kiasi hicho hicho cha mshahara kabla ya mchezaji huyo kukubali uhamisho huo. 
Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho alikuwa radhi kumuacha Torres kabla ya dirisha la usajili kufungwa Jumatatu ili kupata nafasi ya kusajili mshambuliaji mwingine na Loic Remy sasa yupo kwenye nafasi nzuri ya kutua Magharibi mwa London kutoka Queens Park Rangers.

REKODI YA FERNANDO TORRES... 

Atletico Madrid (2001-2007) Mechi 244, mabao 91
Liverpool (2007-2011) Mechi 142, mabao 81
Chelsea (2011-2014) Mechi 172, mabao 45
Timu ya taifa Hispania tangu 2003; Mechi 110, mabao 38

0 comments Blogger 0 Facebook

Chapisha Maoni

ZILIZOSOMWA SANA

 
TASWIRA MICHEZONI © 2015. All Rights Reserved. This Blog Proudly Designed by MMC™ Media Group Ltd | Phone +255-786-758-021
Top